Barua pepe: infokvz@.go.tz  |  S.L.P: 2803  |  Simu: +255 779 569 917


Logo
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar
Logo

Mnamo tarehe 20 Agost,2013

Mhe.Raisi wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein. alifanya mabadiliko ya baadhi ya Wizara ambayo yamepelekea kubadilika kwa miundo ya baadhi ya wizara hizo pamoja na watendaji wakuu.

katika mabadiliko hayo Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serekali za mitaa na Idara maalum SMZ imeundwa rasmi. maeneo makuu ya wizara hii ni:-

A.Mamlaka ya Serikali za Mikoa na Mitaa

B.Vitambulisho vya ukazi sasa inajulikana kama (Ofisi ya usajili wa matukio ya kijamii)

C.Idara Maalumu za SMZ

Pia katiba ya Zanzibar ya 1984 ibara 121 imetoa mamlaka kwa Muheshimiwa Raisi wa Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mapinduzi kuunda Idara maalum ikiwemo Kikosi cha Valantia Zanzibar.

Aidha kwa mujibu wa ibara ya 123(1) kamanda mkuu wa Idara Maalum za SMZ ni Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na waziri wa nchi ofisi ya raisi tawala za mikoa na idara maalum za SMZ ndie msimamizi wa Wizara inayo simamia Idara Maalum za SMZ.

.


DIRA

Dira ya Kikosi Cha Valantia Zanzibar

Kikosi cha Valantia kuwa ni chombo muhimu na chenye ufanisi katika kutoa huduma ya Ulinzi wa Nchi, Raia na mali zao pamoja na kuhamasisha ushiriki wa kiulinzi katika Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

DHAMIRA

Dhamira ya Kikosi Cha Valantia Zanzibar

Ni kutoa Huduma ya Ulinzi kwa kushirikiana na taasisi nyengine za ulinzi na usalama za Serikali ya Zanzibar na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kudumisha Amani na mshikamano wa Taifa. KVZ itajitahidi kutekeleza sera ya Taifa hususa sera ya kupunguza umaskini kupitia sera, mipango na majukumu yake ya kila siku ili kuchangia katika kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa jumla.


Uongozi wa KVZ

Card image
LT COL Said A Juma Shamhuna

Mkuu wa Kikosi Cha Valantia Zanzibar

Wasifu
Card image
MAJOR Juma Hussein Ali

Mkuu wa Utawala wa Kikosi Cha Valantia Zanzibar

Wasifu

© 2021 Kikosi Cha Valantia Zanzibar. Haki zote zimehifadhiwa