Barua pepe: infokvz@.go.tz  |  S.L.P: 2803  |  Simu: +255 779 569 917


Logo
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar
Logo

HUDUMA ZETU

KVZ HOSPITAL
Car
HUDUMA YA AFYA NA TIBA

Ndani ya kvz huduma ya afya zimeanzishwa mwaka 2001. Ilikuwa ni ofisi ya chumba kimoja ambacho ilikuwa kama ni FIRST AIDS iwapo kama askari wanapopata ugonjwa wakiwepo kazini wapate msaada wa mwanzo. Wakati huo huo ofisi za makao makuu yetu ya kikosi yalikuwa maisara wilaya ya mjini kwa kipindi hicho daktari alikuwa mmoja tu muanzilishi..

Jina la sehemu hii inayotoa huduma ya afya ilikuwa na jina la kvz primary health care..

Mwaka 2002 hadi 2007 waliongezeka madaktari 7 na kuwa jumla madaktari 8. Hapo tulianzisha mgawanyiko kwa uhamisho ili kuanzisha huduma hizi na kambi nyengine za kvz nazo ni:-
i. Kambi ya pangatupu
ii. Kambi ya kisakasaka
iii. Kambi ya ndugu kitu pemba

Mnamo mwaka 2010 makao makuu ya kvz yalihama kutoka maisara na kuhamishwa mtoni wilaya ya magharibi “A” tulianza kutanua huduma zetu na tulikiwa na vyumba vitatu (3) ambayo vitatoa huduma kama ifuatavyo:-

a) OPD
b) DRESSING ROOM
c) CHUMBA CHA KULAZWA KWA MUDA (DETAIN)

Jumla ya watendaji wote wa afya katika kituo chetu cha kvz ni 57 na wamegawanyika katika vitengo kama ifuatavyo:-

(1)Madaktari (8)
(2)Wauguzi (23)
(3)Pharmacy (5)
(4)Maabara (5)
(5)Ushauri nasaha (5)
(6)Physiotherapy (3)
(7)Oderly (8)

Watendaji hawa ni mchanganyiko wa askari na raia na wamegawika kwa zamu kituoni na kinafanya kazi masaa 24.

HUDUMA ZINAZOPATIKANA HOSPITALI YA KVZ MTONI

Huduma zinazotolewa:-
1. In and Out Patient (Wagonjwa wa kuingia na kutoka).
2. Laboratory (Maabara).
3. Counselling (Ushauri nasaha).
4. Physiotherapy (viungo).
5. Dental clinic (huduma ya meno).
6. Pharmacy (Utowaji Dawa).

MATARAJIO YETU KATIKA HOSPITALI YA KVZ MTONI

Tunatarajia kutoa huduma nyingine kama zifuatazo:-
i. Kuweka huduma za X-ray na Ultrasound
ii. Kuweka usafiri kwa wagonjwa (ambulance)
iii. Kuweka huduma za mama na mtoto
iv. Kujenga hospital ambayo inaendana na uhalisia wa kidigital
v. Kuongeza madaktari wa fani mbalimbali ambazo kwa sasa hutolewa.
ICT SOLUTION
Car
HUDUMA ZA TECHNOLOGIA YA HABARI NA MAWSILIANO

Kitengo cha Tehama kiliazishwa mwaka 2020 kwa lengo la kuhakikisha miundombinu ya tehama katika kikosi cha valantia Zanzibar inakuwa bora na salama kwa muda wote.

Majukumu ya kitengo cha Tehama katika kikosi cha valantia Zanzibar.

(1) Usimamizi wa mifumo ya kompyuta (system Administration)

(2) Usimamizi wa Mtandao wa kompyuta pamoja na vifaa vyake (network and hadware Administration)

(3) Usimamizi wa Benki ya Takwimu(Database Administration)

(4) Usimamizi wa tovuti na barua pepe (website Administration and email)

(5) Kutekeleza sera ya tehama na serikali mtandao

(6) Matengenezo ya kompyuta(Computer repair and Mantainance)

HABARI NA PICHA - KVZ
Car
HUDUMA ZA HABARI NA PICHA

Kikosi cha valantia Zanzibar ni miongoni mwa idara za idara maalumu zanzibar, mbali na majukumu ya ulinzi wa taifa na kulinda viongozi mbali mbali wa nchi pia kikosi hiki kinatoa huduma mbali mbali kwa askari na raia.

kikosi cha valantia Zanzibar kimeweza kujikita katika harakati za utoaji huduma za habari na picha kiukweli tunao waandishi wa habari waliobobea katika fani hii ya utoaji wa habari ,mbali na utoaji wa habari tuna wataalamu wa kushoot video na wapigaji picha mahiri sana lakini pia wanatoa huduma the video movie burning katika CD karibu kikosini kwetu ili uweze kupata huduma hizi.


© 2021 Kikosi Cha Valantia Zanzibar. Haki zote zimehifadhiwa