Sanaa hujumuisha
Muziki
Ambao unaweza kuwa wa kuimba na wa vyombo uliorekodiwa kwa sauti au utunzi wa muziki ulioandikwa, bendi, muziki wa jazi, ala, uliorekodiwa, video, taarabu, kwaya, gwaride,muziki wa asili wa ngoma na unaoambatana na maigizo na thamthiliya.
Sanaa za Ufundi
Hujumuisha picha za kuchorwa kwa rangi, uchoraji wa kawaida, michoro ya majalada, vitabu au magazeti, uchoraji wa kwenye vitu vigumu kama metali au mbao, uandishi wa herufi ulionakishiwa, sanaa za vikaragosi kwa kutumia kompyuta na michoro iliyochapishwa. Ramani, michoro ya majengo na vielelezo, sanaa za kuumba na kuchonga, picha mgando za kamera, Kazi za usanifu majengo katika maumbo Sanaa za viwandani ikiwa pamoja na zilizo katika picha au zilizofumwa na urembo, na ubunifu wa mavazi, ususi na useketaji wa nguo.
Sanaa za Maonyesho
Michezo ya kuigiza ya jukwaani, maigizo bubu, usanifu wa majukwaa, maleba, mapambo, uandishi wa tamthiliya, ngoma na ubunifu wake, sauti na vifaa vya jukwaani, sarakasi za binadamu au za wanyama, michezo ya redio..