Barua pepe: infokvz@.go.tz | S.L.P: 2803 | Simu: +255 779 569 917
Kikosi cha Valantia Zanzibar kimeanzishwa mwaka 1957 wakati wa harakati za kudai uhuru ambapo vijana wazalendo kwa kushirikiana na chama cha ASP walikuwa miongoni mwao walinzi wa chama hicho.baada ya mapinduzi matukufu miongoni mwa waliojiunga na vikosi vya vya ulinzi na usalama vya SMT na SMZ kama :-
(1)Jeshi la ulinzi la wananchi watanzania (JWTZ).
(2)Usalama wa taifa (TISS).
(3)Polisi.
(4)Kikosi maalumu cha kuzuia magendo(KMKM).
Kipindi chote hicho KVZ ilikuwa inafanya kazi bila malipo na bila sheria hadi mwaka 1982 ikawepo kwa mujibu wa sheria na ikaanzishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 1982 ambapo ilijulikana kwa jina la kikosi maalum cha kujitolea (KMCK).
Ikaendelea hadi mwaka 1992 Tanzania ikaingia katika mfumo wa vyama vingi na kwa kuwa valantia walikuwa katika mfumo wa chama kimoja ,serikali ikaona hakuna haja ya kuwepo kwa valantia.ikaanzishwa rasmi kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mwaka 2004.
Kikosi cha Valantia kuwa ni chombo muhimu na chenye ufanisi katika kutoa huduma ya Ulinzi wa Nchi, Raia na mali zao pamoja na kuhamasisha ushiriki wa kiulinzi katika Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Ni kutoa Huduma ya Ulinzi kwa kushirikiana na taasisi nyengine za ulinzi na usalama za Serekali ya Zanzibar na serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kudumisha Amani na mshikamano wa Taifa. KVZ itajitahidi kutekeleza sera ya Taifa hususa sera ya kupunguza umaskini kupitia sera, mipango na majukumu yake ya kila siku ili kuchangia katika kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa jumla.
Kikosi cha Valantia Zanzibar ni miongoni mwa Idara tano Maalum za Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilicho chini ya Afisi ya Rais Tawala za mikoa na Idara Maalum za (SMZ).
Kikosi cha Valantia Kimeanzishwa Kwa Sheria Namba 5 ya Mwaka 2004 na kwa mujibu wa Sheria hiyo kikosi kina majukumu ya kueka amani na utulivu katika nchi, kupambana na janga lolote litakalo ikumba jamii kulinda Viongozi na mali za serekali na kufanya kazi za kijeshi kwa madhumuni ya kuzuia hali inayohatarisha ulinzi na usalama.
Zanzibar ni mkusanyiko wa visiwa vikubwa viwili vya unguja na Pemba, pia vikipakana pembezoni mwake na visiwa vyengine vidogo vidogo kama Changuu. Misali, Pungume na kadhalika.
Zanzibar ni visiwa vinavyopatikana katika bahari ya Hindi, ni visiwa ambavyo vimebarikiwa neema nytingi hususan matunda na nafaka toifauti, pia ina mandahari nzuri kutokana nafukwe zake pamoja na mji wa kihistoria wa mji mkongwe.
Zanzibar ni mkusanyiko wa visiwa vikubwa viwili vya unguja na Pemba, pia vikipakana pembezoni mwake na visiwa vyengine vidogo vidogo kama Changuu. Misali, Pungume na kadhalika.
Zanzibar ni visiwa vinavyopatikana katika bahari ya Hindi, ni visiwa ambavyo vimebarikiwa neema nytingi hususan matunda na nafaka toifauti, pia ina mandahari nzuri kutokana nafukwe zake pamoja na mji wa kihistoria wa mji mkongwe.
|
KVZ MABINGWA WA FA WAPOKEWA KWA SHANGWE/HAYA HAPA MAPOKEZI YAO NA MAGOLI YAO YA FAINALI FA PEMBA
Kamanda Mkuu wa Kikosi Cha valantia Zanzibar akiwatakia kheri ya mwaka mpya wapiganaji wa KVZ
KWATA YA KIMYA KIMYA IKICHEZWA NA ASKARI WA KVZ KATIKA UFUNGAJI WA KOZI YA LEVEL 03 INT 03 IDARA MAALUM
© 2021 Kikosi Cha Valantia Zanzibar. Haki zote zimehifadhiwa